Saturday, March 8, 2014

HAPPY WOMEN'S DAY LADIES..

Tunawatakia siku hii muhimu ya wanawake duniani, Wanawake ndio kila kitu katika ulimwengu huu, bila wao sijui ingekuwaje... Nawatakia HERI YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI...

Friday, March 7, 2014

Biashara Ikiendelea

Warda akisimamia upakiaji wa bidhaa.

Friday, February 14, 2014

WANAMATU NA BIASHARA

Wanamatu wakiwa busy na kuuza bidhaa zao.. Ahsanteni kwa ushirikiano wenu.






LISHE YA MTOTO

Kwa miezi sita ya kwanza katika maisha ya mtoto chakula pekee ambacho wataalamu wa afya wanashauri apewe ni maziwa ya mama tu. Kunyonyesha ndio njia ya kwanza kabisa kumpa mtoto chakula. Unapoanza kumpa mtoto vitu vingine kama maziwa ya kopo wakati ana miezi michache utoaji wako wa maziwa unaathirika maana jinsi mtoto anavyonyonya ndivyo jinsi maziwa yanavyotengenezwa ndio maana watu wengi wanavyoanza kazi na kumuacha mtoto nyumbani maziwa yao yanaanza kupungua. Faida za kunyonyesha maziwa ya mama ni pamoja na:

Maziwa ya mama yana virutubisho vingi vya asili ambavyo ni muhimu sana katika ukuaji na kinga kwa mtoto. Humlinda na magonjwa mengi ya utoto pamoja na ‘allergies’ mbalimbali.
·       Hukuwezesha kuwa na ukaribu na mtoto wako.
·       Hukupunguzia uwezekano wa kupata kansa ya matiti.
·       Ni bure na unaweza kumpatia maziwa wakati wowote bila usumbufu.





Katika chama chetu kuna biashara nyingi tunazojishughulisha nazo ikiwa ni vikapu vya kina mama, ni vizuri na vinavutia, karibuni sana weka oda yako sasa.
Ahsante.

Thursday, February 13, 2014

Kikundi cha WANAMATU (Wanawake Na Maendeleo Tunaweza) kimeazishwa rasmi Tarehe 8/5/ 2013, ni kikundi ambacho kinalengo la kumuinua mwanamke na maendeleo yake(mfano: sherehe, misiba, ugonjwa na biashara).