Thursday, February 13, 2014

Kikundi cha WANAMATU (Wanawake Na Maendeleo Tunaweza) kimeazishwa rasmi Tarehe 8/5/ 2013, ni kikundi ambacho kinalengo la kumuinua mwanamke na maendeleo yake(mfano: sherehe, misiba, ugonjwa na biashara).



 MADHUMUNI

 A.    Kujikwamua kimaisha katika nyanja zote za kimaendeleo.

 B.     Kusaidiana katika hali na mali, katika taabu na raha na kufanya matendo ya huruma kwa wanajamii wenye mahitaji mbalimbali kama:
(i)       Kuwatembelea wafungwa magerezani wanawake na watoto;
(ii)     Kuwaona yatima na wajane katika shida zao;
(iii)  Kuwafariji wagonjwa mahospitalini;
(iv)  Kutoa ushauri kwa walioathirika na madawa ya kulevya, n.k.



C.    Kuanzisha miradi ya maendeleo yenye lengo la kuhakisha kikundi kina uwezo wa kutekeleza shughuli zake;
                                            i.            Biashara ndani ya kikundi
                                         ii.            Mikopo kwa wanachama



D. Kusaidia /kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii;

E.     Upendo na Mshikamano
                                                        i.            Kushirikiana na vikundi vingine vinavyofanya shughuli kama za kikundi hiki.

F.      Uamini na Uadilifu.

No comments: