Wanamatu wakiwa busy na kuuza bidhaa zao.. Ahsanteni kwa ushirikiano wenu.
Friday, February 14, 2014
LISHE YA MTOTO
Kwa miezi sita ya kwanza katika maisha ya mtoto chakula pekee ambacho wataalamu wa afya wanashauri apewe ni maziwa ya mama tu. Kunyonyesha ndio njia ya kwanza kabisa kumpa mtoto chakula. Unapoanza kumpa mtoto vitu vingine kama maziwa ya kopo wakati ana miezi michache utoaji wako wa maziwa unaathirika maana jinsi mtoto anavyonyonya ndivyo jinsi maziwa yanavyotengenezwa ndio maana watu wengi wanavyoanza kazi na kumuacha mtoto nyumbani maziwa yao yanaanza kupungua. Faida za kunyonyesha maziwa ya mama ni pamoja na:
Maziwa ya mama yana virutubisho vingi vya asili ambavyo ni muhimu sana katika ukuaji na kinga kwa mtoto. Humlinda na magonjwa mengi ya utoto pamoja na ‘allergies’ mbalimbali.
· Hukuwezesha kuwa na ukaribu na mtoto wako.
· Hukupunguzia uwezekano wa kupata kansa ya matiti.
· Ni bure na unaweza kumpatia maziwa wakati wowote bila usumbufu.
Subscribe to:
Comments (Atom)


